Aftatu kuishuhudia Mtibwa, Yanga

3 miezi imepita 37

By  Mwanahiba Richard

Chief Reporter

Mwananchi Communications Limited

Mechi ya Mtibwa Sugar na Yanga inatarajia kuanza kuchezwa saa 10:00 jioni huku mashabiki 3000 pekee ndio wanaoruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi hiyo.

Timu hizo zinakutana kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara inachezwa Uwanja wa Manungu, Turian.

Meneja wa uwanja huo, Godfrey Komba amesema kuwa uwanja wao una uwezo wa kuingiza watu 5000 lakini kutokana na aina ya mashabiki wa timu kubwa Simba na Yanga huwa wanapunguza idadi ya mashabiki kuingia uwanjani.

"Mashabiki wa hizi timu wanakuwa na fujo sana ndio maana tunapunguza idadi kutoka 5000 hadi 3000. Msimu uliopita tuliwaruhusu 2500 kila timu Simba na Yanga, msimu huu tumeongeza kidogo ila hawatavuka hapo,'' amesema Komba

Komba amesema kwa timu zingine zinazokuja kucheza kwenye uwanja wao ni ruhusa kuingiza mashabiki 5000 na sio timu hizo za Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

"Kwa shabiki ambaye atachelewa kukata tiketi basi ataangalizia mpira kwenye televisheni, hataruhusiwa kuingia ndani ingawa mfumo tumeuweka ikifika idadi hiyo hawataweza tena kukata."

Source : Mwanaspoti

SHARE THIS POST