Bodi ya Ligi yataja sababu kupangua ratiba bara

3 miezi imepita 40

By  Charity James

Reporter

Mwananchi Communications Limited

OFISA Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo ametaja sababu saba za kufanya mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Desemba 3 mzunguko wa 19 utamalizika na kufanya idadi ya mechi 152 kati ya 240 pia kutakuwa na kubaki michezo 88 kumaliza ligi ya msimu huu.

Kasongo amesema wamefanya mabadiliko kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo ushiriki wa timu tano za Tanzania Bara katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza rasmi Januari mosi 2023.

“Kuna sababu saba ambazo tumeamua kufanya maboresho ya ratiba ya Ligi Kuu, ikiwemo kombe la  Mapinduzi, imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi, tunatambua mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika michezo na tumeamua kufanya mabadiliko kwa sababu ya timu tano kutoka Bara kwenda kucheza michuano hiyo,"

Sababu ya pili kuhusu Timu yetu ya Taifa Stars kuhusiana na michuano ya CHAN, yatajayofanyika nchini Algeria,  katika ratiba yetu ya awali tuliweka timu yetu kufika mbali na kuipa nafasi lakini imeondolewa hivyo ratiba ikalazimika kufanyiwa maboresho,” amesema Kasongo.

Ameeleza sababu zingine ni michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika na Ligi ya Mabingwa, kwa Yanga na Simba kwa kuwapa nafasi klabu hizo kujiandaa na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza mwezi Febuari.

“Wamewaondolea mechi za karibuni ambazo wanatakiwa kucheza mwezi huo na kuwapa muda wa timu hizo kujiandaa vizuri kuelekea michuano hiyo ya Kimataifa kwa sababu ni wakilishi pekee Tanzania,"

Mabadiliko hayo pia imezingatia Taifa Stars kuelekea michuano ya AFCON, tukiwa na mechi mbili nyumbani na ugenini dhidi ya Uganda, mchezo huo utapigwa kati ya Machi 20 hadi 28, 2023,” anasema Kasongo.

Amesema kuelekea michuano hiyo Taifa Stars inatakuwa kuingia kambini mapema kwa ajili ya michezo hiyo lakini pia ratiba hiyo imezingatia uwepo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inaendelea na sababu zingine za mikataba hasa kwa Azam TV.

“Febuari 12, na  Mei 19 hadi 25 , itakuwa wiki ya kombe la Shirikisho kwa raundi tano, kwa kuchezwa mzunguko wa 32, 16, robo na nusu fanali.

Sababu ya mwisho  za kikanuni kabla ya corona kushamili, ligi kucheza Agosti hadi Mei, hali hiyo ikafanya mabadiliko na sasa tunahitaji kurejea katika utaratibu wa awali kwa mzunguko Wa mwisho utacheza utachezwa tarehe moja (Mei 28, 2023, kwa timu zote kucheza muda mmoja,” alisema Mtendaji huyo.

Anasema Kuna mambo mengi yametokea katika, Bodi ya Ligi  kwa kushirikiana na  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamekaa na kwa lengo la kufanya mabadiliko ya ratiba ya ligi ili kuakisi michuano iliyopo mbele kwa timu ya taifa na klabu.

“Niwashukuru wadhamini ambao tunafanya nao kazi kwa mchangao wao katika kutumiza yale ya kimkataba ambayo tumekubaliana, wadhamini watatu tuliokuwa nao ndio wanafanya timu zetu kuweza kusafiri na kufanya mambo mengine ya kufedha”, anasema Kasongo.

Source : Mwanaspoti

SHARE THIS POST