DC Apson atembelea miradi ya ujenzi wa madarasa

2 miezi imepita 44

Apsoni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo amefanya ziara hiyo jana katika shule ya Sekondari Kilingi inayonjengwa madarasa matatu, shule ya sekondari Magadini inayojengwa madarasa matatu na ofisi moja ya walimu, shule ya Sekondari karansi madarasa matatu na nyumba moja ya waalimu, shule ya Sekondari Nuru madarasa mawili na ofisi moja ya walimu pamoja na shule ya Sekondari Esinyari madarasa mawili.

Kwa mujibu wa Apson amesema hivi karibuni Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliipatia fedha Halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 480, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 24 vya madarasa .

Hata hivyo, Apson amewashauri mafundi wanaoendelea na ujenzi wa madarasa hayo kujitahidi kwenda na kasi ya ujenzi inayotakiwa lakini kwa ubora unaostahili.

Source : Nipashe

SHARE THIS POST