02Dec 2022

Shufaa Lyimo

Nipashe

Ihefu SC, Kagera kibaruani Ligi Kuu

WAKATI kikosi chake kikijiandaa kuifaa Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa leo, Kocha Mkuu wa Ihefu SC, Juma Mwambusi, amesema anahitaji kusajili wachezaji wapya wawili ili kuiongezea nguvu timu yake.

Kocha Mkuu wa Ihefu SC, Juma Mwambusi.

Mwambusi aliliambia gazeti hili nyota hao wapya wakipatikana wataziba nafasi ya ushambuliaji na umaliziaji ambazo zimeonekana kuwa na mapungufu msimu huu.

"Safu ya umaliziaji ina mapungufu, mara nyingi wachezaji wangu wanapata mipira lakini wanashindwa kufunga, inanipasa nifanye usajili mzuri ili kuhimili ushindani," alisema Mwambusi.

Kocha huyo alisema mastraika wake wanakosa utulivu wanapofika katika lango la wapinzani na kupelekea kupoteza michezo iliyopita ya ligi hiyo.

Aliongeza amejipanga vizuri kuwakabili Kagera Sugar na anaamini wachezaji wake wataendelea kujituma kusaka ushindi na kujiondoka kwenye nafasi waliyopo kwenye msimamo.

Habari Kubwa

  • Majeneza yenye miili ya wanafamilia waliofariki kwa ajali ya gari, Immaculata Byemerwa (mama) na watoto wake, Janeth Byemerwa na Jolista Byemerwa, yakiwa kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Tabata Kuu jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya ibada kabla ya kusafirishwa kwenda Kibaha mkoani Pwani kuzikwa. PICHA: JUMANNE JUMA