01Dec 2022

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM

Nipashe

Iptisum Slim apata A, matokeo darasa la saba

Mwanafunzi wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary iliyopo mkoani Pwani, Iptisum Slim, aliyebadilishiwa namba ya mtihani wa darasa la saba amefaulu kwa wastani wa alama A.

Sakata la Iptisum liliibuka Oktoba 14, baada ya kusambaa kwa video akiomba msaada kwa serikali, akihofia kupoteza haki yake ya kusoma, baada ya kupewa namba 39 ya mhitimu mwingine badala ya namba yake halali 40.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alitangaza kufanya uchunguzi, kuiifungia shule hiyo ya iliyopo mkoani Pwani kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana.

Leo Alhamisi,  Desemba 01, 2022 Kaimu Katibu Mtendaji NECTA, Athumani Salumu ametangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba, yanaoonesha Iptisum amefaulu kwa wastani wa A, kwa kupata alama A katika masomo manne na B katika masomo mawili.

Masomo aliyopata A ni Kiswahili, English, Maarifa na Sayansi huku aliyopata B ni Hisabati na Uraia.

Habari Kubwa

  • Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, akideki barabara pamoja na vijana wa mkoa wa Lindi.