Jinsi ajali za barabarani zinavyosababisha vifo vya watu nchini 

2 miezi imepita 35

Kwa kipindi cha miaka minne kuanza 2017 hadi 2020 jumla ya watu 7537 walifariki  kutokana na ajali za barabarani hiyo ni sawa na kusema kuwa kila mwezi watu takribani 157 wanapoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.

Mbali na watu kupoteza maisha ajali hizo zimekuwa zikiacha maelfu ya majeruhi wamepata ulemavu wa muda na wa kudumu ulio sababishwa na ajali  au kupata tatizo linalo walazimu kuopatiwa matibabu hospitali kwa kipindi kirefu .

Katika ripoti ya polisi ya hali ya uhalifu na usalama barabarani kwa kipindi cha miaka minne miongoni mwa vyanzo vya ajali vinavyo bainishwa   ni sababu za ki binadamu kama mwendo kasi ,ubovu wa vyombo vya usafiri, na sababu za kimazingira kama ubovu wa barabara,vizuizi,ulevi,uzembe wa madereva pikipiki,mikokoteni ,baiskeri na watembea kwa miguu.

Mwaka 2017 Ripoti hiyo inabainisha  sababu za ki binadamu zilichangia ajali kwa asilimia 81.1%,Sababu za ubovu wa vyombo vya moto  zilichangia kwa asilimia 8.9% huku sababu za kimazingira zikichangia kwa asilimia 10.0%  

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo ajali zinazo sababishwa na sababu za kibinadamu kwa miaka minne mfululizo zina ongezeka kila mwaka kwani 2018  ilifikia  87.9% mwaka 2019  asilimia 91.2% na mwaka 2020 ilipanda hadi kufikia asilimia  91.6% hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 10.5 kwa kipindi cha miaka minne .

Mnamo mwezi Julai  mwaka huu waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni aliagiza jeshi la polisi kuhakikisha linasimamia vyombo vya usafirishaji wa abiria kwenye kutumia vyema mfumo wa vidhidibiti mwendo (VTS) kama hatua ya kupunguza ajali.

Ambapo alibainisha kuwa kuna na baadhi ya wamiliki wa magari wanao chezea mfumo huo kwa lengo la kuendesha magari kwa kasi pasipo kubainika  ambapo kwa mujibu wa ripoti ya hali ya uhalifu na usalama barabarani inayotolewa na jeshi la polisi mwaka 2017 mwendokasi ulichangia ajali kwa asilimia 7.4%,mwaka 2018 ilikua aslimia 9.1%,mwaka 2019 asilimia  9.8% huku mwaka 2020 ikiwa  asilimia 10.7% hii ikiwekwa miongoni mwa sababu za kibinadamu.

Akitoa mfano wa ajali iliyotokea Morogoro na kusababisha watu 22 kupoteza maisha alisema endapo gari hilo lingekuwa na ubora madhara ya idadi hiyo ya watu kupoteza maisha yasingefikia kiwango hicho hivyo jeshi la polisi linapaswa kuboresha ukaguzi wa magari utakao saidia kuepusha madhara zaidi.

Kutokana na vyanzo vya ajali vinavyo  tajwa kwa kipindi cha miaka minne zikionesha asilimia za sababu za kibinadamu kuzidi kuongezeka katika  kusababisha ajali barabarani  kuna haja ya serikali kuongeza nguvu ya utoaji elimu kwa watumiaji wa barabara ili kukumbushwa mara kwa mara  matumizi sahihi na kuepukana na makosa ambayo yangeweza kuzuilika.

Source : Nipashe

SHARE THIS POST