Kadogosa afunguka mabehewa ya TRC yaliyokuwa yapigwe mnada "Treni zilizoahidiwa na zilizokuja"

1 wiki imepita 29


Shirika la Reli Nchini (TRC) limesema mabehewa yote yaliyoanishwa kuletwa kwa ajili ya treni ya Reli ya Kisasa (SGR) yatakuja na kwamba yaliyoanza kuingia nchini ni za safari ndefu. Wiki hii katika mitandao ya jamii kumekuwa na picha zikionyesha mabehewa yaliyoletwa sio yale yaliyoahidiwa kuletwa nchini kutokana na tofauti ya muonekano wake. Hayo yamesemwa leo Alhamis Novemba 24, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea ujenzi wa SGR katika eneo la Kikuyu jijini hapa
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST