31Dec 2022

Shufaa Lyimo

DAR E SALAAM

Nipashe

Kitila mgeni rasmi Kombe la Ubungo

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Kitila Mkumbo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya fainali ya mashindano ya Kombe la vijana la Wilaya ya Ubungo ( UFa CUP) itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Mabomba FC watakutana na Makuburi katika mechi hiyo ya fainali ambayo mshindi atazawadiwa Sh. 300,000 pamoja na jezi na mipira miwili.

Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA), Frank Mchaki, alisema awali fainali hiyo ilipangwa ifanyike tangu Septemba, mwaka huu lakini iliahirishwa kutokana na msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wao, Benjamin Mwakasonda.

Mchaki alisema maandalizi ya fainali hiyo yako katika hatua za mwisho na mshindi wa pili atapata zawadi ya Sh. 100,000.

Aliwataka vijana kutoka sehemu mbalimbali wajitokeze kushuhukia mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani.

Habari Kubwa

  • Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi.

  • aliyekuwa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah.