KLABU YA ROTARY DAR  YAKABIDHI MADAWATI 300 SHULE YA MSINGI KUNDUCHI

2 miezi imepita 25

Na.Khadija Seif, Michuzi TV

KLABU ya Rotary Dar es salaam imekabidhi Madawati 300 yenye thamani ya Shilingi Milioni 38 kwa shule ya Msingi Kunduchi Jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa Kukabidhi Madawati hayo Leo Aprili 01,2023 Jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amesema Serikali inathamini jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Klabu ya Rotary Dar kwa kuendelea kutoa misaada ya Madawati pamoja na vitabu kuhakikisha wanafunzi mashuleni wanajifunza katika Mazingira rafiki.

"Wadau hawa wamekuwa msaada mkubwa kwa Wilaya ya Kinondoni na inania ya dhati kuwa inahitaji shule za wilaya hii kuendelea kufanya vizuri na kuongoza Kiwilaya na hata Kimkoa kwa natokea ya mitihani ya ngazi zote."

Hata hivyo Mtambule ameongeza kuwa Wilaya ya Kinondoni inaendelea kufanya vizuri katika masomo na Dar es salaam kuongoza namba 1 kwa mwaka 2022 kwa shule zilizofanya vizuri mtihani wa darasa la 7 hiyo yote ikichangiwa na Mazingira kuboreshwa na wadau kama Klabu hiyo.

Pia ametoa wito kwa wanafunzi hao kuhakikisha Madawati hayo yanatunzwa vizuri ili vizazi vijavyo wayatumie Madawati hayo na kuwaomba Klabu hiyo kuendelea kutoa madawati kwa shule zingine zenye changamoto.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Klabu ya Rotary Dar Ezra Kavana amesema Klabu ya Rotary Dar lengo lake kubwa ni kusaidia wanafunzi mashuleni kwani wanafunzi hao ndio viongozi wa baadae pamoja na wataalam mbalimbali wanazaliwa huko hivyo ni muhimu kukawa na matayarisho ya viongozi hao kuanza Mazingira pamoja na nyenzo bora za kufundishia.

"Idadi ya Madawati ambayo Klabu yetu yameshatoa ni takribani Madawati 2,300 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 300 ambapo madawati haya yanaenda kuondoa tatizo la uhaba wa Madawati shuleni hapo na hivyo kuanzia sasa Wanafunzi wote wa shule hiyo watakuwa wanakaa kwenye Madawati ambapo awali shule hiyo ilikua ikikabiliwa na changamoto ya Madawati 300."

Nae Mkuu wa Shule ya Kunduchi Moses Amani ametoa shukrani zake kwa uongozi wa Klabu hiyo kwa msaada wa Madawati hayo ambapo ilikua ni changamoto ya shule hiyo kwa muda mrefu.

"Shule yetu ilikua ikikabiliwa na changamoto ya Madawati kwa muda mrefu, tulikuwa tukifanya Ukarabati kwa Madawati yaliopo lakini mwisho wa siku yamekuwa machakavu zaidi hivyo Madawati haya yamekuja wakati sahihi "

Hata hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia kujenga vyumba vya Madarasa 24, matundu ya choo 24 na kuomba kujengewa uzio shuleni hapo. kwani kuna wanafunzi 2665 ni wengi hivyo hata mahitaji huongezeka .

Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Kampuni ya SBC Tanzania kupitia kinywaji cha pepsi Foti Gwibe Nyirenda amesema wataendelea kuwaunga Mkono Klabu ya Rotary Dar katika harakati zao za Kuhakikisha wanatengeneza Miundombinu rafiki kwa wanafunzi Mashuleni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizungumza machache na kuwasisitiza wanafunzi kutunza Madawati hayo ambayo wadau wa elimu Klabu ya Rotary Dar imekuwa ikitoa kwa shule mbili lengo ni kuimarisha miundombinu bora mashuleni.

Mjumbe wa Kamati ya Klabu ya Rotary Dar Ezra Kavana  akizungumza na Wanahabari Leo Aprili  01,2023 mara baada ya kukabidhi rasmi Madawati 300 yenye thamani ya Shilingi Milioni 300 ikiwa ni muendelezo wa Klabu hiyo kutoa misaada Mashuleni.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kunduchi  Jijini Dar es salaam Moses Amani akizungumza na Wanahabari Leo Aprili 01,2023 wakati alipokabidhiwa Madawati 300 yenye thamani ya Shilingi Milioni 38 na Klabu ya Rotary Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Kampuni ya SBC Tanzania kupitia  kinywaji cha Pepsi  Foti Gwibe Nyirenda amesema wataendelea kuwaunga Mkono Klabu ya Rotary Dar  katika harakati zao mara kwa mara.Picha ya Pamoja ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kunduchi iliyopo Tegeta Jijini Dar es salaam Pamoja na Uongozi wa Klabu ya Rotary Dar ikiongozwa na Rais Nikita Arragawal, Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka SBC Tanzania Foti Gwibe Nyirenda wakati wa kumalizika kwa zoezi la ugawaji wa Madawati

Source : Michuzi Blog

SHARE THIS POST