Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba,Wampongeza Rais Samia

1 wiki imepita 17


MADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na kufikia 16 hali ambayo imeendelea kuifanya Tanzania kuwa kivutio cha utalii tiba Kusini mwa Jangwa la Sahara. Madaktari hao walikuwa India kwa siku 10 wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tifa Taifa, ambaye ni Mkurugenzi wa Global Education Link na Global Medicare, Abdulmalik. Mollel alipewa ruhusa na Mwenyekiti wake, Profresa Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, (MNH) kuongozana na ujumbe huo . Hayo yalisemwa jana jijjini Dar es Salaam na daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mgongo wa taasisi hiyo, Nicephorus Rutabasibwa, wakati akizungumza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Terminal III. Alikuwa akizungumza wakati yeye na madaktari bingwa 10 waliporejea kutoka India ambapo walikwenda kutafuta fursa za kushirikiana na hospitali mbalimbali za nchini humo ikiwa ni jitihada za kukuza utalii tiba hapa nchini. Alisema waliangalia nguvu ya Tanzania katika matibabu na kwamba hawakukuta tofauti sana kwani vifaa tiba na rasilimali watu ya madaktari iliyoko kule ni kama iliyoko hapa nchini.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST