Maganga alivyombananisha Katambi leo "Niseme kabisa mheshimiwa Waziri sijaridhika na majibu haya"

1 wiki imepita 25


Mbunge wa Mbogwe Nicodemus Maganga amehoji serikali kuwapiga chenga wastaafu pindi wanapoanza kudai mafao yao. Akiuliza swali la msingi, Maganga amehoji Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha pesheni za wastaafu zinalipwa kwa wakati?. Akijibu swali hilo leo Ijumaa Mei 26, 2023 Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi, amesema kuwa mifuko inaendelea kuimarisha mifumo ya ndani ya ulipaji wa mafao ili kuhakikisha maombi ya wastaafu wapya yanafanyiwa kazi kwa haraka.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST