Mbowe afunguka sababu za CHADEMA kutosambaratika," Wengine wameunga juhudi"

1 wiki imepita 28


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ameitaka Serikali kutotumia mabavu kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi badala yake hekima itumike ikiwemo kutoa elimu na ushirikiashwaji ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo ikiwemo migogoro ya ardhi. Pia amesema Chama hicho kitaendelea kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia maridhiano ili kuhakikisha changamoto zinazowatesa Watanzania zinatatuliwa. Ametoa kauli hizo alipokuwa akihutubia wakazi wa Katavya Usevya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara wa Operesheni +255 Katiba Mpya huku akisisitiza kwamba pamoja na ushirikiano huo wataendelea kudai Katiba Mpya ambayo ni mwarobaini wa kudumu wa changamoto hizo.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST