Mkasa Wanigeria watatu kujificha kwenye rada uvunguni wa meli siku 11

2 miezi imepita 22

Kwa njia hiyo, hatimaye serikali ya Uhispania ilitoa ruhusa kwa meli kuondoka bandarini, ikiwaacha wahamiaji watatu kwenye kisiwa cha Gran Canaria.

Pia ilithibitishwa shirika lisilo la kiserikali la Caminando Fronteras, liliitaka mamlaka kusimamisha kurejeshwa kwa wahamiaji hao watatu wa Nigeria.

"Ukweli wa kupitia safari ya hatari kama hiyo inapaswa kuzingatiwa kama dalili ya kuchambua kibinafsi hali ya kibinafsi ya waathiriwa watatu," ilitamka asasi hiyo katika taarifa yake, ikionya kwamba wahamiaji wawili walikuwa wamehamishwa kurudi kwenye meli siku ya Jumanne.

Vile vile, walikuwa wameomba kukaribishwa katika mojawapo ya vituo vya wahamiaji "ili wapate usaidizi unaohitajika wa kutulia kiakili na kisaikolojia kwa kuzingatia hali ya matukio na safari ya hatari ambayo inaweza kuwa mbaya."

ILKUWAJE?

Jinsi walivyofikia rada ya usukani haijulikani. Kinachojulikana ni kwamba Wanigeria hao watatu walizamia meli hiyo katika bandari ya Lagos, Nigeria, kabla ya Alithini II yenye bendera ya Malta. kuanza safari mnamo Novemba 17.

Safari ya kuelekea kisiwa cha Gran Canaria ilidumu kwa siku 11 mfululizo. Mnamo Jumatatu, Novemba 28, Salvamento Marítimo aliwaokoa baada ya kufaulu kufika Las Palmas, baada ya kuonekana katika sehemu ya chini ya meli.

Mahali walipopatikana ni nafasi iliyoko kwenye kile kiitwacho rada au usukani wa nje ya sehemu ya meli, ambayo huwa wazi na inaweza kushambuliwa na pigo lolote kutoka baharini.

Picha iliyosambaa kwa kasi duniani ilipigwa na mlinzi wa chombo cha uokozi ya Salvamar Nunki, Orlando Ramos Alayón, ambaye aliwaokoa.

"Ni kawaida. Huwa tunachukua picha hizo ili kuzihifadhi kama kumbukumbu," Orlando Ramos anaeleza katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano.

"Ni muhimu kuokoa maisha ya watatu hao, na wengine ambao hufika uhamishoni bila nguvu, wakiwa wadhaifu, na kuathiriwana baridi kali."

"Kulikuwa na wanaume watatu kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara waliokuwa wadhaifu baada ya kuathiriwa na baridi kali. Watu wawili kati ya waliokolewa walipelekwa katika Hospitali … na yule aliyekuwa katika hali mbaya zaidi alisafirishwa hadi Hospitali ya Insular," inasema taarifa kutoka meli hiyo.

Wawili kati yao waliachiliwa muda mfupi baadaye na kurudishwa kwenye meli ya mwanzoni, lakini baadaye walitolewa tena kwenye meli hiyo baada ya kuomba hifadhi.

Mwathiriwa wa tatu bado amelazwa hospitalini, ambako anaendelea kupata matibabu kutokana na upungufu wa maji mwilini, maisha yake hayako tena hatarini, kulingana na mamlaka.

"Ni sehemu ambayo mtu hawezi kukaa, ukizingatia hali ya mazingira ya bahari kuu mtu anaweza kufa kutokana na upungufu wa maji mwilini, kuanguka ndani ya maji kutokana na dhoruba ya bahari.

“Upepo ni mkali unaosababisha hypothermia ... ni hatari kubwa. Eneo hilo linaweza kujaa maji. Kuna uwezekano mkubwa wa hili kutokea, "inaeleza taarifa.

Hasui sasa inaeleza, mamlaka inayosimamia uokoaji imerekodi mikasa mitano kama hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

Mnamo Januari 2018, Salvamar Nunki iliokoa watu wanne kwenye meli ya Green Sky waliokuwa wamejificha kwenye rada.

Mnamo Oktoba 2020, wazamiaji wanne walipatikana kwenye gurudumu la meli ya mafuta ya Norway ya Champion Pula, baada ya kusafiri kutoka Lagos hadi Las Palmas.

Mwezi huo huo, Salvamar Nunki iliokoa 7 kwenye rada ya meli ya Andromeda.

Mwezi mmoja baada ya operesheni hiyo, mnamo Novemba, mashua hiyo hiyo iliokoa mtu aliyekuwa amejificha kwenye rada.

Hadi kufika Juni mwaka huu, shirika lisilokuwa la kiserikali la Caminando Fronteras lilisajili vifo 800 kwa namna hiyo na mwaka jana Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) lilirekodi vifo 1,532 katika njia hiyo.

  • Kwa mujibu wa taarifa kimataifa.
  • Ends

Cap

 Sehemu ya chini walikojificha wazamiaji hao. PICHA: MTANDAO.

Source : Nipashe

SHARE THIS POST