Mshindi wa promosheni ya NMB MastaBata KoteKote akabidhiwa pikipiki

2 miezi imepita 31

Washindi 49 walijishindia pesa taslimu Sh. milioni 1 kila mmoja na wawili wakishinda pikipiki aina ya Boxer.

Lengo la kampeni hii ya MastaBata KoteKote ni kuhamasisha matumizi ya kadi ya NMB Mastercard na Lipa Mkononi (Mastercard QR) kwa wateja wetu wanapofanya malipo kwenye manunuzi yao.

Mkazi wa Bunda jijini Mara, Bernard Lucas Matiku alisema: "Asante sana Benki yangu ya NMB kwa kunizawadia pikipiki, nimeanza vizuri msimu huu wa sikukuu maana sasa sina wasiwasi kuendesha mishe zangu" Hiyo ni kauli ya mshindi baada ya kukabidhiwa pikipiki yake.

Zoezi hilo lililosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania limepelekea idadi ya washindi wa kampeni ya NMB MastaBata KoteKote kufikia 225 hadi sasa.

"Zawadi walizoshinda wateja hao kwa siku hii zina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 55 huku shindano zima likiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni 300," 

"Zawadi za kila wiki zitakuwepo ambapo jumla ya washindi 75 watanyakua pesa taslimu Sh. 100,000 kila mmoja na mmoja zawadi ya pikipiki (boxer), kwa mwezi jumla ya washindi 98 watanyakua pesa taslimu Sh. milioni 1 kila mmoja huku kila mwezi kukiwepo zawadi ya pikipiki (Boxer) mbili.

"Zawadi ya droo ya mwisho ni safari ya siku nne huko Dubai kwa washindi saba na wenza wao.Endelea kufanya malipo kwa kutumia NMB mastercard au Lipa Mkononi (mastercard QR) ujiwekee nafasi ya kushindia zawadi kibao na #NMBMastaBataKoteKote.

Mshindi wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku(wa pili kushoto) akibonyeza kitufe ili kuwapata washindi wengine wa kampeni hiyo. Wakishuhudia; Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi wa NMB- Philbert Casmir, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka Ladislaus(wa tatu kushoto) na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha - Erick Mremi(kulia).

Source : Nipashe

SHARE THIS POST