MSUKUMA APIGA KIINGEREZA BUNGE LAAMKA AULIZA MASWALI MAGUMU SPIKA TULIA AOKOA JAHAZI

2 wiki zimepita 62


Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma akiuliza swali kwa Kiingereza kwa mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki Mhandisi Mohamed Mnyaa wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Baada ya Spika Tulia Ackson kumtaja Musukuma kuuliza swali kwa mgombea huyo, wabunge wameibua shangwe na kugonga meza huku baadhi wakimtuza fedha kutokana na umahiri wake wa kuulizwa swali kwa lugha ya kiingereza. Mbunge Musukuma amemuuliza Mnyaa kuwa "kwa kipindi cha miaka mitano amefanya nini mpaka aombe tena kuchaguliwa katika Bunge hilo?." Hata alivyotakiwa kurudia tena swali hilo bado Mbunge huyo alikua na ujasiri na kuuliza. Mara kadhaa Mbunge Musukuma amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema elimu yake ni darasa la saba, lakini ana uwezo mkubwa kulinganisha na wale wanaojiita wasomi.
Source : Bongo5

SHARE THIS POST