Mtibwa yaitangulia Yanga

3 miezi imepita 39

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Communications Limited

Manungu. MTIBWA Sugar ndiyo ilikuwa ya kwanza kuingia kwenye uwanja wa Manungu wakiingia saa 14:08 huku Yanga wakiingia saa 14:24 mchana.

Timu hizo zinatarajia kucheza mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kuanzia saa 10:00 jioni ambapo mechi ya mzunguko wa kwanza ilichezwa Uwanja wa Mkapa na Mtibwa kupokea kichapo cha mabao 3-0.

Timu hizo kila mmoja inaonekana kuhitaji zaidi pointi tatu ambapo Yanga inataka kujiimarisha kilele mwa msimamo wa ligi kwani sasa ina pointi 47 wakati Mtibwa wana pointi 24.

Wakati timu hizo zinawasili upande wa Mtibwa aliyekuwa wa kwanza kushuka ni Meneja wa timu Henry Joseph na upande wa Yanga alikuwa ni Aziz KI.

Timu zote ziliingilia geti moja ambalo hutumiwa na magari pamoja na mashabiki na ziliingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo moja kwa moja kabla ya kwenda kupasha uwanjani.

Source : Mwanaspoti

SHARE THIS POST