g

Saa 2 zilizopita

Maelezo ya video,

'Nalazimika kuuza ng’ombe kununua chakula cha ng’ombe wengine' – Wanawake wa Kimaasai Kenya

Wanawake wa Kimaasai nchini Kenya wanapiga picha kuhusu jinsi ukame unavyoathiri riziki ya maisha yao.

Shirika lisilo la faida limewapatia kamera kwa ajili ya kuhifadhi mabadiliko yaliyosababishwa na ukame mbaya kuwahi kushuhudiwa kwa miongo.  

Wanawake wa Amboseli wanachukua picha za mabadiliko ya tabia nchi , kama vile kulazimika kuwalisha mifugo wao unga kwasababu nyasi zimenyauka.