Ntibazonkiza apewa Prisons

3 miezi imepita 44

By  Eliya Solomon

Reporter

Mwananchi Communications Limited

SUPASTAA Saidi Ntibazonkiza amepewa shavu la kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ambacho muda mchache ujao kitacheza dhidi ya Mafaande wa Tanzania Prisons kwa Mkapa.

Nyota huyo ambaye amejiunga na Simba akitokea Geita Gold  kwa mkataba wa miaka miwili wakati wa dirisha hili la usajili hii itakuwa mara yake ya kwanza kuwatumikia wekundu hao wa Msimbazi.

Licha ya ugeni wake, kocha wa Simba, Juma Mgunda ameamua kumtishwa mabomu mshambuliaji huyo ili aongoze safu yake sambamba na John Bocco.

Ntibazonkiza ambaye aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kwenda Geita  anatazamwa kama mchezaji ambaye anaweza kuongeza makali kwenye safu hiyo ya ushambuliaji kutokana na kukosekana kwa Moses Phiri ambaye ni majeruhi.

Kikosi kamili cha Simba kinaundwa na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Joash Onyango, Hennock Inonga, Sadio Kanoute, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, Bocco, Ntibazonkiza na Pape Sakho.

Source : Mwanaspoti

SHARE THIS POST