Ongezeko vitendo ulawiti watoto linavyochangia athari za kijinsia

2 miezi imepita 33

Hiyo inajidhihirisha kupitia Ripoti ya Jeshi la Polisi ya kila mwaka kuhusu matukio yaliyo ripotiwa  katika jedwali la makosa ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.Ifuatayo ni idadi ya matukio ya watoto walio lawitiwa nchini Tanzania  yaliyotolewa taarifa polisi kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2017,2018 ,2019 na  2020 .

Kwa mwaka 2017 watoto 501 mwaka 2018   1,159 sawa na ongezeko la watoto 658 , mwaka 2019 watoto  1,405 ni  ongezeko la watoto 246 uki linganisha na mwaka 2018 huku  mwaka 2020 idadi ya vitendo hivyo vikipungua na kuripotiwa watoto waliotendewa ukatili huo kuwa  ni 257.

Kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2017 hadi 2020 takribani matukio ya watoto kulawitiwa  3,322 yaliripotiwa polisi huku asilimia 86 kati yao wakiwa watoto wa kiume sawa na idadi ya  2,885 sawa na wastani wa kila mwezi watoto wa kiume  60 wana fanyiwa ukatili huo.

Ukiangalia takwimu hizo utabaini watoto wa kiume wako kwenye hatari zaidi ya kutendewa unyanyasaji huo kwani kwa kipindi cha miaka minne kati ya watoto walio lawitia wa kiume ni asilimia 86 hivyo kuna haja ya hatua za haraka kuchukuliwa ili kuwalinda watoto husussani wa kiume.

Taarifa hiyo inaonesha namna ukatili huo unavyo athiri jinsia zote hasa hali ikiwa mbaya zaidi kwa kundi la watoto wa kiume ambao idadi yao inaonesha kuwa juu zaidi ya wa kike.

Ripoti ya takwimu za hali ya uhalifu na matukio ya usalama barabarani  zinabainisha miongoni mwa vichocheo  vya ukatili huo ni utandawazi ,ukosefu wa maadili ya kidini na jamii, tamaa za kimwili na imani za kishirikina kwamba zimekuwa ziki sababisha mwendelezo wa ukatili huo

Mwanasaikolojia kutoka Hospitali Kanda ya Rufaa ya Mbeya, Idara ya Afya  ya Akili, kitengo cha saikolojia tiba, Yisambi Ndagamsu  anasema mtoto aliyelawitiwa ana athiriwa na hisia ,fikra na kitabia.

Kadri mtoto anavyo endelea kukua na kubaini  alicho fanyiwa hakiendani na tamaduni inasababisha kujitenga ,kuona hafai na anaweza chukua maamuzi ya kujitoa uhai kwa kuwa na hisia za kuwa hana tena thamani na anaweza pata ugonjwa wa Sonona

Ndagamsu anasema miononi mwa athari za watoto kufanyiwa hivyo husababisha kufikia uraibu ambao awali wakiwa wanatendewa ukatili huo uumia lakini baadayehuitaji kuendelea ku fanywiwa mara kwa mara .

‘’Nimepata kesi kadhaa kushauri watu wanao vutiwa na mapenzi ya jinsia moja lakini wengi wao nikiongea nao nina baini waliwahi kutendewa vitendo hivyo na kushindwa kupata matibabu haraka’’Anasema Ndagamsu.

Anawashauri wazazi kujenga urafiki na watoto ili pindi wanapo tendewa ukatili huo waweze kubaini mapema na kuwasaidia matibabu yatakayo wawezesha kuachana na vitendo hivyo na kutokufikia kwenye uraibu.

Hatua muhimu za  kumsaidia mtoto alietendewa ukatili ni lazima kubaini chanzo cha tabia hiyo endapo ni  nyumbani,shuleni au marafiki wanao kaa na mtoto ,hiyo husaidia  kupata suluhisho la kudumu na kumsaidia kuachana na tabia hiyo.

"Nina shauri ukiona mtoto katendewa ukatili huu fika kwa wataalamu wakusaidie namna nzuri ya kumsaidia pasipo kumuumiza na kusababisha afikie uraibu"anasema Ndagamsu.

Kutokana na kukithiri kwa ukatili wa kingono kwa watoto jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limeendelea kuinua kiwango cha uelewa wa jamii na kuimarisha huduma ya Madawati ya Jinsia katika vituo vya polisi ili kuhamasisha wananchi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto hatua itakayo wezesha kubaini ukubwa wa tatizo na kutafuta suluhisho katika udhibiti.

Source : Nipashe

SHARE THIS POST