01Dec 2022

Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam

Nipashe

PSSSF yatwaa tuzo ya umahiri katika uwasilishaji taarifa za mahesabu

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa Tuzo ya Umahiri katika Uwasilishaji wa Taarifa za Mahesabu kwa mwaka 2021, kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Tuzo hiyo iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Beatrice Musa-Lupi katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam usiku wa Novemba 30, 2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Ikulu, Serikali yaMapinduzi Zanzibar, CPA. Jamal Kassim Ali.

PSSSF imetwaa tuzo hiyo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021(Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa mwaka wa pili mfululizo.

Akizungumza kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba, amesema tuzo hiyo itaongeza chachu kwa watumishi wa PSSSF katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na hivyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa Mfuko.

Aidha, Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Beatrice Musa-Lupi amesema ushindi huo ni ishara ya kwamba PSSSF inaandaa mahesabu kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa lakini pia inaashiria uwepo wa weledi wa tasnia husika kwa upande wa watumishi.

Habari Kubwa

  • Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, akideki barabara pamoja na vijana wa mkoa wa Lindi.