Sababu maambukizi ya UKIMWI kukithiri Mkuranga yatajwa

2 miezi imepita 33

Hayo yalisemwa na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Gamasu Sogosogo, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.

Maadhimisho hayo yalifanyika kikaka, katika viwanja vya Shule ya Msingi Mipeko na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali, likiwamo shirika lisilo la kiserikali la Himiza Development Organization.

"Tangu Januari hadi Oktoba mwaka huu, watu 2165 walipima VVU, 51 waligundulika kuwa na maambukizi, huku wanaume wakiwa 14, wanawake 37," alisema Gamasu.

Ofisa Mtendaji huyo aliongeza kusema; " Sababu kubwa ya kuwapo kwa maambukizi mwingiliano wa watu unaotokana na kuwapo kwa viwanda katika kata yetu.'

Alitaja sababu nyingine kuwa ni watu kutozingatia elimu kuhusu kujikinga na ugonjwa huo, tabia hatarishi majumbani ikiwamo ukatili wa ngono, ulevi kupindukia na ngoma za usiku.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mwezeshaji wa kitaifa wa afya ya akili, msaada wa kisaikolojia na kijamii kutoka TAMISEMI, Leokadia Mbawala, alisema serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha biashara ya ngono inatokomeza.

"Ungeni mkono juhudi za serikali, ikibidi, kila mmoja arudi katika imani yake ya dini na kubadili tabia, ili kukabiliana na ugonjwa huu hatari," alisema Leokadia.

Aidha, aliwataka wale ambao wanatumia dawa za kufubaza VVU kutokatiza dozi, badala waendelee kutumia.

"Lakini jamii nayo isiwanyanyapae wanaotumia hizo, kwani wengine wamekuwa wakiziacha kutokana na kunyanyapaliwa majumbani na mitaani," alisema.

Alisema jamii ikiungana katika vita dhidi UKIMWI, maambukizi yanaweza kuisha, kwa kuwa kila mmoja atakuwa anajua wajibu wake.

Source : Nipashe

SHARE THIS POST