Simanzi !!! Mwili wa askofu wakutwa ukielea majini

2 miezi imepita 30


Mwanza. Jeshi la Paolisi Mkoa wa Mwanza limethibisha kupatikana kwa mwili wa Askofu mstaafu wa kanisa la Aglikana Diocese ya Victoria Nyanza, Boniphace Kwangu (61) uliokutwa ukielea ndani ya maji kando ya ziwa victoria karibu na eneo linapojengwa daraja la JPM (Kigogo- Busisi). Taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Ijumaa Desemba 2, 2022 inasema, asubuhi ya Novemba 28, 2022 eneo la Shibula Wilaya ya Ilemela Askofu huyo aliaga familia yake na kuelekea wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya Sh2.5 milioni baada ya kuuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT- Sengerema.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST