Waziri awawakia Vigogo wanaoacha kazi za ofisi na kupambana na mambo yao binafsi

2 wiki zimepita 38


Waziri wa Madini Dk Dotto Biteko amejikuta akiwa mkali kwa watendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini GST huku akiwataka watendaji wake watakapoondoka na kuiacha taasisi hiyo kuacha utafiti utakaosaidia wachimbaji wadogo nchini kunufaika na utafiti mpya na kuachana na ule wa zamani ambao unatumika hadi sasa hivi. Waziri Biteko ameyasema hayo leo Septemba 23, 2022 wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) huku akieleza kukasirishwa na baadhi ya watendaji wa bodi ambao wamekuwa wakihangaika na majukumu yao na kuwa na dharura nyingi na kusahau majukumu ya GST
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST