Waziri Mkuu aridhishwa na maendeleo ya ujenzi SGR

1 wiki imepita 31


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha mradi huo unajengwa kwa viwango na kukamilika kama ilivyo bainishwa kwenye mkataba. Amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri katika vipande vyote na kwamba Serikali itahakikisha mradi huo haukwami na itakabiliana na viashiria vyote vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wake. Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 24, 2022) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni kuu ya Dodoma katika eneo la Mkonze, jijini Dodoma. Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo wasimamie usalama wa mradi na wawe walinzi ili ukamilike kama ilivyokuwa.
Source : Mwananchi Digital

SHARE THIS POST