Wizara ya mifugo yakanusha kupiga marufuku Taa za Sola kwenye uvuvi wa dagaa Ziwa Victoria

3 miezi imepita 54


Mkurugenzi wa Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Magese Bulayi amekanusha taarifa iliyosambaa kwenye vyombo vya habari kuwa wizara imesitisha matumizi ya taa za nishati ya jua “Taa za sola” zinazotumia betri za pikipiki katika uvuvi wa dagaa kwenye Ziwa Victoria kuanzia Januari mosi 2023. Mbali ya kukanusha huko Bulayi ameongeza kuwa wavuvi wa Ziwa Victoria wanapaswa kupuuza taarifa hizo na kuendelea na shughuli zao kwa kutumia zana na njia rafiki zinazolinda rasilimali za uvuvi. #AzamTVUpdates #WavuviZiwaVictoria #TaaZaSola #UvuviSalama
Source : AzamTV

SHARE THIS POST