Wizara yakanusha taarifa ya kusitishwa Kwa matumizi ya taa za Sola
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekanusha taarifa iliyosambaa hivi karibuni ya kusitishwa kwa matumizi ya Taa za Sola zinazotumia betri za pikipiki katika Uvuvi wa Dagaa kwenye Ziwa Viktoria kuanzia Januari Mosi 2023 huku ikiwataka wavuvi hao kuendelea na shughuli zao kwa kutumia zana na njia rafiki zinazolinda rasilimali za Uvuvi. Kanusho la Serikali limetolewa jijini Dodoma Disemba 31, 2023 na Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Magese Bulayi ambapo ameeleza kuwa agizo la kusitisha matumizi ya taa hizo ni madai yasiyo na ukweli wowote hivyo wavuvi wa dagaa katika ziwa Victoria wanapaswa kupuuza na kuendelea na majukumu yao.