Yanga yamaliza mwaka kibabe, Azizi Ki bado hajamaliza

3 miezi imepita 47

Jumamosi, Desemba 31, 2022

By  Mwanahiba Richard

Chief Reporter

Mwananchi Communications Limited

Summary

  • Bao la Stephane Aziz Ki limeihakikishia Yanga pointi tatu wakiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo wa Ligi Kuu NBC uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

MTIBWA Sugar imeshindwa kuipunguzia mlima Simba wa kufikia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kukubali kipigo dhidi ya Yanga ambao sasa wamefikisha pointi 50.

Kabla ya mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Manungu, Yanga walikuwa na pointi 47 huku Simba wakiwa wamesogea kwa kufikisha pointi 44 sasa wamezidiwa pointi sita huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 19.

Aziz KI aliyefunga bao la kwanza dakika ya 27 amefikisha mabao matatu hadi sasa huku akionekana kuwa mwiba kwa wachezaji wa Mtibwa Sugar.

KI alifunga bao hilo kwa mpira wa faulo huku dakika ya 45 pia akikosa bao la pili baada ya kupiga shuti ambalo lilidakwa na kipa wa Mtibwa Sugar,  Razack Shekimweri. Ki alipiga mpira huo wa faulo katika eneo lile lile alilopiga faulo ya kwanza iliyozaa bao.

Kipindi cha pili Mtibwa walionekana kubadilika na kumiliki zaidi mpira ingawa safu yao ya umaliziaji ilishindwa kufunga pale waliopata nafasi huku Kipa wa Yanga, Diarra naye alikuwa imara kwenye kupangua hatari zilizoelekezwa kwake.

Shekimweri alikuwa na kibarua cha kupangua mashuti ya Aziz Ki kabla hajafanyiwa mabadiliko na kuingia Geay Bigirimana dakika ya 80 pamoja na Jesus Moloko aliyetoka na kuingia Dickson Ambundo.
Kocha wa Yanga Nassredine Nabi alimtoa Farid Musa nafasi yake ilichukuliwa na David Bryson pamoja na Tuisila Kisinda/ Clement Mzize
Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga naye alifanya mabadiliko ili kukipa uhai zaidi kikosi chake ingawa mabadiliko hayo hayakumsaidia katika kusawazisha bao hilo.
Mayanga aliwatoa Ismail Mhesa/Onesmo Mayaya na Omary Sultan/Joseph Mkele ambao waliingia kwa pamoja dakika ya 81.


REKODI ZAO KATIKA MICHEZO 10 ILIYOPITA KATI YA YANGA NA MTIBWA SUGAR

-Yanga 3-0 Mtibwa Sugar (Septemba 13, 2022)
-Yanga 1-0 Mtibwa Sugar (Juni 29, 2022)
-Mtibwa Sugar 0-2 Yanga (Februari 23, 2022)
-Yanga 1-0 Mtibwa Sugar (Februari 20, 2021)
-Mtibwa Sugar 0-1 Yanga (Septemba 27, 2020)
-Mtibwa Sugar 1-1 Yanga (Julai 22, 2020)
-Yanga 1-0 Mtibwa Sugar (Februari 2, 2020)
-Mtibwa Sugar 1-0 Yanga (Aprili 17, 2019)
-Yanga 2-1 Mtibwa Sugar (Agosti 23, 2018)
-Mtibwa Sugar 1-0 Yanga (Mei 13, 2018)

Katika michezo hizo 10, Yanga imeshinda saba wakati Mtibwa Sugar imeshinda miwili na sare mmoja.,

Kwenye michezo hiyo Yanga imefunga mabao 13 wakati Mtibwa Sugar imefunga manne tu.


VIKOSI

Mtibwa Sugar: Razack Shekimweri, David Kameta, Issa Rashid, Jofrey Luseke, Vedastus Mwihambi, James Kotei, Ismail Mhesa/Joseph Mkele (Dak 81),  Balama Mapinduzi,  Charles Ilanfya, Juma Ganambali na Omary Hassan/Onesmo Mayaya (Dak 81).

YANGA: Diarra, Kibwana Shomary, Farid Musa, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Zawadi Mauya, Jesus Moloko/Dickson Ambundo (dakika ya 80), Salum Abubakar,  Fiston Mayele, Aziz KI/Geay Bigirimana (Dak 80) na Tuisila Kisinda.

Source : Mwanaspoti

SHARE THIS POST