Zaidi ya kaya 200 kupatiwa Mbuzi bure Handeni
Zaidi ya kaya 200 halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga zinatarajiwa kunufaika na mradi wa kupewa mtaji wa Mbuzi ambazo zinatolewa bure lengo likiwa ni ili ziweze kujimudu kiuchumi. Hayo yameelezwa na muwakilishi wa taasisi ya Islamic Help wilaya ya Handeni Habibu Mbota wakati wa kukabidhi mradi huo wa Mbuzi kwa uongozi wa kata ya Malezi na kueleza kuwa utawanufaisha wanawake wajane.